BAADA YA MAANDAMANO.
Imeamdaliwa: GLEN DON
Katiba humu nchini inaruhusu kuwepo kwa maandamano ila iwe maandamano ya amani yasiyo na uchochezi, ghasia wala uhalifu.
Leo ni siku ya tatu ya maandamano tangu Mheshimiwa Raila Odinga kutangaza maandamano hayo kufanyika mara tatu kwa wiki mfululizo ikiwa ni; Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.
Maandamano hayo ni ya kupinga bajeti ya mwaka wa fedha ya 2023/24 na pia kushinikiza serikali kupunguza gharama na hali ya maisha magumu yanayokumba wananchi.
Bwana Odinga anahisi kuwa serikali inafanya kazi duni kupunguza gharama ya maisha.
Njia hii ya maandamano ilibuniwa na wanasiasa wa Azimio wakiongozwa na Bwana Odinga ili kufikisha ujumbe nzito kwa serikali.
Tangu maandamano hayo yaanze, serikali haipinduki wala hawatikiswi, je tunaweza sema kuwa maandamano hayana ujumbe au ni serikali kichwa ngumu na haitaki kusikiliza malalamishi ya wananchi?
Bwana Odinga ni miongoni mwa shujaa ambao walitetea sana hapo awali demokrasia, ustawi wa uchumi, na pia kuwepo huru nchini Kenya.
Iweje baadhi ya maendeleo haya leo yanapitia majaribu mikononi mwa waandamanaji.
Kila siku ndani ya waandamanaji kuna wale wachochezi, wahalifu, na wenye tendo la ugaidi vilevile kuna wale waandamanaji halali wale wanaoandamana juu ya hali gumu ya maisha, pia kuna wale wanao tii sheria na kauli za Bwana Odinga kwani 'Baba' akisema kulia au kushoto ni hivyo.
Kila mara watu wanapo andamana lazima wawe watu hawa watatu.
Mioto zinawakizwa barabarani, mali kuharibiwa kama ile tukio ya Mlolongo Machakos, uporaji wa mali kwa hali ya utata, kando na hayo maisha yanapotezwa.
Tangu maandamano yaanze inakadiriwa kuwa vifo vya watu isiyopungua 30 vimetokea na makumi ya watu kuumia kutokana na ghasia ya maandamano, cha kutikitisha ni kuwa mauaji na majeraha haya yanasababishwa na wanapolisi, Swali ni Je Serikali inatumia nguvu kupita kiasi au ni waandamanaji Wana ugumu wa kuelewa jukumu lao wanapo andamana? Pengine ni vibaya kukata hukumu shingo upande, na tusitumie mate wino ungalipo.
BAADA YA MAANDAMANO
Tunapochoma lami na kupora mali ya Wakenya wenzetu, je tumezika wapi fikra zetu?
Lazima tujue kuna maisha baada ya maandamano.
Barabara zinapochomwa na mali zinapoporwa ni taswira mbaya tunayoonyesha.
Kuna njia mbadala ya kuashiria ghadhabu tunapoandamana.
Tunapo washa moto kwenye barabara zetu, ni maendeleo tunarejesha nyuma, tunapo pora mali ya Wakenya wenzetu ni chuki tunaeneza.
Sisi ni Wakenya wazalendo, katika wimbo wetu wa taifa tunahimizwa kupitia wimbo huo, kuwa tuishi kwa amani, na tunapotenda matendo yanayokinzana na mistari za wimbo wetu wa taifa, je huo ni uzalendo?
Kwa hakika, maandamano yamekubaliwa na katiba yetu, pia panapofanyika maandamano viongozi huwa hawana amani na wanaibishwa mno, Kwa hivyo wazo la fikra ni je Bwana Ruto anaweza kimya tu hivyo anapoona hayo yote yakifanyika?
Kuna Maisha baada ya maandamano.
Kuna amani baada ya maandamano, ndiyo tunafaa kudumu ndani ya upendo na umoja.
Tunapoeneza chuki, swali tunalofaa tujiulize kimawazo ni, je jirani wangu kesho ataweza kuniazimu maji ya kunywa, ata tone tu la kuua tama? Je nitaweza kusafiri popote nchini kwa amani? Ninasisitiza kuwa kuna Maisha baada ya maandamano.
Yaliyojengwa miongo kadhaa tusiyabomoe kwani kuna maisha ya kuishi baada ya maandamano na tutayategemea. Tusibomoe daraja baada au kabla ya kuvuka bahari kwani kesho pia ni siku.
Tusiwadharau mashujaa waliopigania uhuru wa taifa letu, waliopigania uchumi wetu. Kazi nzuri waliofanya tusije tukayazike.
Njia bora ni kulinda kazi waliozifanya kwa kuwa kuna maisha baada ya maandamano.
Idadi kubwa ya waandamanaji ni vijana, na wazee ni nadra sana kupata.
Tunavyojua ujana ni moshi, na uzee hauepukiki, kesho tukisha zeeka, tutaambia wajukuu na watukuu nini?
Tutawaambia nini, ikiwa tunazungumza lugha moja na hakuna amani, upendo na umoja? Ikiwa maendeleo hayatakuwa na fursa tulikuwa nazo sote?
Kuyajenga yaliyoharabiwa kwa hakika si rahisi,
Maandamano ya mwaka huu si ya kwanza, ya hapo awali maafa yalitokea na haki ingali kutimizwa, pia tukumbukeni kuwa maisha yaaja mara moja na hayawezi kukarabatiwa wala marejesho hayako.
Tutamlilia nani aje ajenge barabara, tutapata wapi pa kustawisha biashara zetu siku zijazo.
Kuna Maisha baada ya maandamano.
Wakati majirani wetu wanaendelea kufanya kazi nasi tupo barabarani keshoye ikifika tutasema nini wakitucheka.
Tunayo maisha baada ya maandamano na ni jukumu letu kuweka maisha hayo yawe ya maana na dhamana.
KUNA MAISHA YA KUISHI.
Kila siku tujue ya kwamba " maji mtoni hayasubiri mwenye kiu."
Kwa: WANANCHI WAZALENDO
EAGLE'S 🦅 EYE 👁️ (JICHO LA TAI)
Comments
Post a Comment